Utani huu wa JPM mmmmmh Download mp3 - Download video

Share
Add
 • Published on Sep 13, 2018

 • ONA HII "BREAKING NEWS: MAMIA WAFARIKI BAADA YA LORI LA MAFUTA KUANGUKA NA KULIPUKA" https://www.youtube.com/watch?v=Ti60g... --~-- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 12 Septemba, 2018 amewaapisha viongozi watatu aliowateua hivi karibuni. Viongozi walioapishwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Dkt. John Kiang’u Jingu, Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz Ponary Mlima na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP Diwani Athumani Msuya. Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Satano Mahenge. Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Jingu kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufuatilia usajili na utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), na kuhakikisha yanafanya kazi kwa kuzingatia sheria ambazo pamoja na mambo mengine zinayataka kuendesha shughuli zao kwa uwazi hususani masuala ya mapato na matumizi ya fedha za ufadhili wa shughuli zake. Mhe. Rais Magufuli amemtaka Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Mlima kusimamia vizuri ushirikiano wa Tanzania na Uganda hasa biashara na uwekezaji unaoendelea kati ya nchi hizi mbili na kuhakikisha Tanzania inanufaika na ushirikiano huo. Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Diwani Athumani Msuya kuongeza kasi ya kushughulikia tatizo la rushwa nchini kwa kuhakikisha wote wanaokabiliwa na tuhuma za kujihusisha na rushwa wanafikishwa mahakamani na sheria inachukua mkondo wake. Mhe. Rais Magufuli pia amemtaka CP Diwani kuungalia upya muundo wa TAKUKURU ili uweke bayana majukumu ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, na kuhakikisha watendaji wa taasisi hiyo wanaoonekana kutofanya kazi kwa tija na kujihusisha na vitendo vya rushwa wanachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa kazini na kufikishwa mahakamani. “Nataka ukaisafishe TAKUKURU, kuna baadhi ya wafanyakazi wa TAKUKURU wanajihusisha na rushwa, kawaondoe, nataka kuona TAKUKURU inashughulikia rushwa kwelikweli hasa rushwa kubwakubwa, ukipita huko vijijini wananchi wanateseka sana, wananyanyaswa na kuna dhuluma nyingi sana, na tatizo kubwa ni rushwa” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli. Viongozi walioapishwa na Mhe. Rais Magufuli pia wamekula kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela na baada ya viapo vyao wamemshukuru Mhe. Rais kwa kuwateua na wamemuahidi kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.
 • Utani huu wa JPM mmmmmh tags

Comments

 • Edson Laurence Mwagamasasi

  Ndio maana nakukubali Sana your Excellency Head of the State President John Pombe Magufuli

 • Magesa Samweli
  Magesa Samweli 6 months ago

  Kaka .Nilikuwambia kuwa Mungu Anaonyesha Kwa Vitendo Usihofu Haki haipotei Tazama Mwenyewe uwezo WA mungu

 • photoshoping with MgoliMusa

  💥💥NJOO UONE JINSI MTU ANAGEUZWA KWENYE MAUMBO MBALIMBALI BONYEZA. PROFILE PICHA YANGU HAPO KUSHOTO 👈

 • Magesa Samweli
  Magesa Samweli 1 week ago

  Diwani Athumani Umeona Mungu Anavyo Simamia Haki Mimi Na sema Hivi Mungu Aku Tangulie sana

 • Paschal Wzychalz
  Paschal Wzychalz 1 year ago

  Hongera Raisi wetu na Mungu akulinde na kukupa nguvu na akuongoza katika hila zote mbaya akupe wepesi na akuepushe dhidi ya mwovu ibilisi kwan nashetan nae yupo kazin asiyekukubali huyo nae ni jipu anasubiri kukamuliwa Salute kwako Babuu

 • Idrisa Petto
  Idrisa Petto 8 months ago

  Pccb temeke ndiyo ichunguzwe jamani

 • FRIDOM GREVAZI
  FRIDOM GREVAZI 1 month ago

  hat waliomsaliti gaddafi saivi washmkumbuka

 • Ephraim Ndelwa
  Ephraim Ndelwa 1 year ago

  Hakika historia yako mh Jpm hazitaandikwa na sisi wanadam, tutakubeza tu! Ila naamini nia yako ya dhati kulikomboa taifa hili ni Mungu pekee ndo ataiandika historia yako haitafutika kamwe kama mfalme daudi

 • timothy ngeleja
  timothy ngeleja 1 year ago

  That's good, God bless Tanzania

 • Jaqline Mwampashe
  Jaqline Mwampashe 5 months ago

  head of state of God congre to you jpm

 • Rajabu Muhode
  Rajabu Muhode 1 year ago

  Usipomkuali leo basi atakapostaaf kazi utamkumbuka tu tena mengi yaliyomema

 • John Lenatus
  John Lenatus 5 months ago

  Safi tungepata maraisi kama hawa watatu tungefika mbali

 • Wited Steward
  Wited Steward 9 months ago

  Jamani sipendi chama cha ccm ila kiongozi wetu rais wetu wanch anayoyafanya nimakubwa makubwa makubwa sijawahi ona mungu azidi kukupa uelekeo wakutosha najua si watu wengi wanao kupenda ila mm nasema unayoyafanya sidhani kuna kiongozi mwingine anayeweza kuyafanya :::: mungu bariki kiongozi wangu, mungu bariki raisi wanch ya Tanzania, mungu mpe uwezo wakuendesha nchi hii kwa uadlilifu, mungu bariki Dk JOHN POMBE MAGUFULI amina

 • ARTIST KIM
  ARTIST KIM 1 year ago

  Hongera rais wetu tunazidi kukuombea kwa mungu azidi kukupigania

 • Safari Mallya
  Safari Mallya 10 months ago

  Shikamooo Baba

 • Ritha Mdakie
  Ritha Mdakie 1 year ago

  Mungu ataendelea kukulinda ktk utendaji wako wa kazi

 • Hydan Adolf
  Hydan Adolf 1 year ago

  yani kweli Raisi ninaye anayejali na kuona yajayo na naamini kuwa yajayo yanafurahisha na ni mazuri zaidi

 • Mshindi Victor
  Mshindi Victor 6 months ago

  Nakuelewa baba

 • halima mbwego
  halima mbwego 11 months ago

  Nakupenda rais wangu

 • Emmanuel Mkeba
  Emmanuel Mkeba 11 months ago

  Nampenda sana huyu Raisi analeta Uzalendo, Uwajibikaji, kujituma, kazi madhubuni na hofu ya Mali za umma wa Watanzania tuko nyuma yako nitakuunga mkono hata Kama ningekuwa kiongozi chama pinzani nami ningejiudhuru wanaojihudhuru wengi wametuona sisi Wananchi tumekukubari wangi wanahofu especially wapinzani kutokurudi 2020 tutaandamana nchi nzima kutaka uongoze miaka 50